Mafunzo ya uongozi na usimamizi wa fedha yafanyika kwa klabu za waandishi wa habari.
viongozi wa iringa press club wakiwa katika mafunzo ya uongozi na usimamizi wa fedha
 Viongozi wa iringa press club wakiwa katika mafunzo ya  uongozi na usimamizi wa fedha

Mafunzo  ya Uongozi na Usimamizi wa fedha yanaendelea katika klabu zote za Waandishi wa Habari Tanzania.

Mafunzo hayo yana lengo la kutoa maelekezo kwa viongozi wa klabu za waandishi wa habari nchini, namna bora ya kutunza na kusimamia matumizi ya vifaa na rasilimali fedha  kwa faida ya klabu na wanachama wake .

Pia mafunzo hayo yamelenga kuongeza uelewa wa namna klabu za waandishi wa habari zitakavyo toa huduma bora kwa wadau wa habari ili kuharakisha maendeleoa yao binafsi na mkoa kwa ujumla .

Klabu ambazo tayari zimepatiwa mafunzo mpaka sasa ni pamoja na Mwanza , Mara, Simiyu, Pemba,  Zanzibar, Mbeya,  Iringa,  Mtwara, Ruvuma,  Lindi  , Arusha, Tanga, Central , Shinyanga,  Dar es Salaam na Morogoro .

Mafunzo haya yanatolewa kwa viongozi wa ngazi za juu wa Klabu ambao ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu,  Kaimu Katibu Mkuu,

Mwekahazina  na Mratibu wa klabu.

Katika mafunzo haya miongozo miwili imetengenezwa  ambayo  ni  Mwongozo wa Kanuni  na Taratibu za  Matumizi ya Fedha na Mfumo wa Uandishi wa Vitabu vya Hesabu kwa Klabu za Waandishi wa Habari, pamoja na Mwongozo wa Klabu za Waandishi wa Habari wa Namna ya Kutoa Huduma kwa  Wadau.

Miongozo hii imeanza kutumika rasmi na klabu zote za Waandishi wa Habari  Tanzania ambazo zimeshapewa mafunzo.

 

Picha zaidi za mafunzo mikoani

{phocagallery view=category|categoryid=19|limitstart=0|limitcount=0}

Recommend to friends
  • gplus
  • pinterest